Mkuu wa Wilaya ya Muheza Bi Subira Mgallu
(Picha na Maktaba)
|
BAADHI ya Wakuu wa Idara wilayani Muheza, Tanga, wamemlalamikia
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amiri Kiroboto, kuwa amekuwa akitumia magari
kinyume na taratibu hali inayowafanya washindwe kufanyakazi zao kwa wakati.
Akizungumza na tovuti ya Fullshangwe kwa njia ya simu juzi, kwa masharti
yakutoandikwa jina lake gazetini, mmoja wa Wakuu wa Idara hizo, alisema, Sheria
za Tamisemi zinasema siku za kufanyakazi kwa wenyeviti wa Halmashauri zote
Tanzania ni mbili ambazo ni Jumatau na Alhamisi, labda kama inapotokea dharula
nje ya siku hizo.
Alisema mwenyekiti huyo amekuwa akifika ofisini kila siku kama vile
watendaji wengine na kuamua kuchukua gari la Idara kama ni elimu au yeyote na
kuondoka nalo pamoja na dereva anakojua hali inayokwamisha shughuli za
watendaji husika pindi wanapotaka kulitumia gari husika kikazi.
Mkuu huyo wa Idara, alisema Mwenyekiti huyo, amekuwa akiyatumia magari
hayo hata siku za mapunziko kwa matumizi yake binafsi kama vile kwenda nayo
katika mashamba yake ya Kwarubuye, Kivindo na Mwarimba, huku madereva wakilipwa
na halmashauri hiyo.
Alisema kuwa, mwenyekiti huyo, amekuwa akitumia lita 80 za mafuta
hadi 100 kwa wiki ili hali alitakiwa kutumia lita 20 katika siku mbili hizo
alizopangiwa, ambazo ni kumfuata nyumbani na kumpeleka kazini na kumrudisha.
Alipotafutwa, Kiroboto ili kutoa ufafanunuzi kuhusu tuhuma hizo, alisema,
hao wamekosea kwa sababu kama kweli hilo lipo basi lilikuwa linazungumzika
lakini kama wamekimbilia huko basi huo ni utashi mdogo wakutoelewa taratibu za
kazi.
“Hayo madai si sahihi, tayari tumeishaingia katika kipindi kigumu cha
uchaguzi sasa watu wanatafuta sababu yakunichafua kupitia katika matumizi
mabaya ya magari kitendo ambacho nilikikwepa kwa muda mrefu hata hivyo mimi
nina magari yangu ambayo ndiyo ninayoyatumia kwenye shughuli zangu,”alisema
Kiroboto.
Kiroboto, lisema hayo ni majungu katika sehemu za kazi, wanapaswa kujua
kuwa kunawakati anakuwa na kazi za dharura, sasa wanapomuona na gari la
Halmashauri basi wajue kuwa yuko kazini na si vinginevyo kama wanavyodai.
No comments:
Post a Comment