Na Mwandishi Wetu Pwani.
JESHI la Polisi Mkoa
wa Pwani linamshikilia Mhandisi Msose Michael (35) mkazi wa Mkaongo Juu Dar es
Salaam, kwa tuhuma za kuwalawiti mabinti wawili katika Kijiji cha Zogowale
wilayani ya Kibaha.
Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoa huo, Athumani Mwambalaswa alithibitisha kukamatwa kwa mhandishi
huyo na kusema aliwalawiti mabinti hao wenye miaka 12 na 16 kwa nyakati
tofauti.
Alisema mtuhumiwa
huyo aliwachukua mabinti hao kutoka Nachingwea kwa nyakati tofauti na kukaa nao
nyumbani kwake jijini Dar es Salam kwa ajili ya kufanya kazi za ndani.
Alisema baada ya
siku kadhaa, aliwahamishia kwenye shamba lake lililopo Zogowale kwa ajili ya
kutunza mifugo yake na kwamba alikuwa akilala nao chumba kimoja pindi
alipowatembelea.
Kwa mujibu wa
kamanda huyo, wananchi walioshuhudia kitendo hicho walitoa taarifa polisi ambao
waliweka mtego na kumnasa mtuhumiwa huyo.
“Baada ya mtuhumiwa
huyo kuwekwa chini ya ulinzi, mabinti hao ambao walipelekwa katika kituo cha
afya Mlandizi kupimwa na kugundulika kwamba walilawitiwa hivyo kuanzishiwa
matibabu,” alisema kamanda huyo.
No comments:
Post a Comment