Na Lodrick Ngowi.Mwanza
ZAIDI
ya wafanyabiashara 600 wakubwa na kati wa jijini Mwanza,
wametangaza mgomo mkubwa usio na kikomo unaotarajiwa kuanza kesho
ukiwa na lengo la kupinga kodi lukuki pamoja na mizigo yao kukamatwa
na Halmashauri ya Jiji.
Akizungumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Umoja wa
Wafanyabiashara jijini hapa, Christopher Wambura, alisema maamuzi hayo
yalifikiwa juzi katika kikao cha pamoja kati ya wafanyabiashara na
mameneja wa biashara wa matawi ya benki ya CRDB jijini.
“Tumeamua kugoma pasipo kikomo hadi kero zetu zitatuliwe,
tulishawasilisha malalamiko yetu kwa Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikillo
ili tukutane na mkurugenzi wa jiji, lakini mpaka sasa hakuna
lililofanyika,” alisema Wambura.
Alisema wafanyabiashara wa Mwanza wameitisha mgomo huo kutokana na
kutosikilizwa kilio chao kikiwemo kutozwa ada za leseni, tozo
mbalimbali, kukamatwa mizigo yao nay a wateja.
Aidha, Wambura alisema kero hiyo ya inayofanywa na jiji, inasababisha
kuwapoteza wateja wanaonunua mali katika maduka huku machinga
wanaofanya biashara mbele ya maduka na kuzuia wateja, wakiachwa.
“Wafanyabiashara tumejitahidi kuwasiliana na viongozi wa mkoa akiwamo
mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na mkurugenzi, lakini hakuna juhudi
zozote ambazo zimefanyika kupitia viongozi hao…tumeamua kudai haki
kupitia mgomo,” alisema.
Alisema katika kikao hicho walichofanya juzi, umoja wao uliazimia
kutofungua biashara zao kwa siku zisizofahamika ili kushinikiza tatizo
lao liweze kutatuliwa.
Wambura alisema kodi wanazotozwa bila mpangilio na tozo nyingine
mbalimbali pamoja na mizigo yao kukamatwa na ile ya wateja wao
waliyoinunua.
Alisema: “Kumekuwa na uonevu wa kutunyang’anya mizigo yetu pamoja na
wateja wetu pia, lakini mali hizo hazifahamiki wapi zinaenda…pia haki
ya kufanya biashara kulingana na kodi tunazolipa haziendani kutokana
na machinga kupanga mbele ya milango ya maduka yetu.”
Mgomo huo kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza utakuwa wa tatu baada
ya ule wa Desemba mwaka jana na Februari mwaka huu, iliyokuwa ikipinga
matumizi ya mashine za kielekroniki (EFDs) za Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA).

No comments:
Post a Comment