MWAFRIKA MWINGINE AUAWA NCHINI MAREKANI
Mauaji mengine
ya raia wa kiafrika yaliyofanywa na polisi katika eneo la St Louis yameongeza
hali ya wasiwasi na vurugu katika eneo hilo ambalo kwa takriban siku 11 sasa
kumekuwa na vurugu kutokana na mauaji yaliyotokea awali.
Jumanne wiki hii afisa mmoja
wa polisi alimpiga risasi na kumuua raia wa kiafrika aliyedaiwa kuwatishia kwa
kisu polisi.Mkuu wa polisi wa St Louis Sam Dotson amesema mauaji hayo ya August 9 ya Michael Brown yameongeza hali ya machafuko katika eneo hilo.
Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder anatarajiwa kutembelea eneo la Ferguson jumatano wiki hii ili kujadili taaerifa rasmi za uchunguzi wa mauaji hayo.
Mwendesha mashitaka katika kesi ya mauaji ya ya Michael Brown leo amewasilisha ushahidi dhidi ya afisa anayedaiwa kuhusika katika mauaji ya Michael Brown.
Vurugu zimeendelea katika mji huo huku waandamanaji wanaopinga mauaji hayo wakiwa wamepakaa maziwa usoni kujikinga na mabomu ya machozi kufuatia waandamaji wawili kuathirika na mabomu hayo.
James Enzi na Uhai wake akiwa kazini |
HUZUNI KUBWA MWANAHABARI AUWAWA
NCHINI SIRYA
Kikosi cha
kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji
ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu
alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa
ameuawa.
Katika mtandao wa kijamii wa Facebook familia ya mwandishi huyo iliandika kuwa’tunajua kwamba wengi wenu mnasubiri uthibitisho ama majibu ya maswali yenu,tafadhalini muwe watulivu mpaka nasi sote tupate taarifa tunazo tamia,na tunaomba muendelee kumbumbuka Foleys na kumwombea kila siku.’’
Katika video hiyo iliyobeba ujumbe unaosomeka kua ujumbe kwa Marekani,mwandishi huyo pia alionekana akiwa chini ya ulinzi wa mtu aliyekua amevalia kinyago usoni,askari huyo alikua aku akizungumza ndani ya lafidhi yenye athari za Uingereza,akisema kua kifo cha mwandishi huyo ni matokeo ya mashambulizi ya magurunedi yalowalenga wa Iraq.
MAROKETI MATATU YARUSHWA KUTOKA GAZA
Israel imefanya mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza hivi leo, huku Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, akiwaamuru wajumbe wa nchi yake kwenye mazungumzo ya amani mjini Cairo kurejea nyumbani. Taarifa ya serikali imesema Netanyahu ameamuru mashambulizi hayo kufanyika katika kile alichokiita kujibu maroketi yaliyorushwa kuelekea Israel hivi leo
Hapo kabla, jeshi la Israel liliripoti kwamba maroketi matatu yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza na kuangukia kusini mwa Israel hapo jana, ikiwa ni masaa kadhaa kabla ya usitishaji wa mapigano na wanamgambo wa Kipalestina kumalizika.
Msemaji wa jeshi amesema maroketi hayo yameangukia katika eneo la wazi karibu na mji wa Beersheba na hakuna ripoti za watu waliojeruhiwa ama kuuwawa.
Mapema mwakilishi wa Palestina kwenye mazungumzo ya Cairo,Azzam al-Ahmad alionya kwamba muda wowote ghasia zingerudi upya kwenye Ukanda wa Gaza kutokana na kusuasua kwa juhudi zao za kufikia makubaliano ya kudumu katika mazungumzo hayo yanayosimamiwa na Misri.
SOMALIA :MMOJA WA WATUHUMIWA WAKUU WA UHARAMIA AKAMATWA.
Vyombo vya usalama nchini Somalia vimedai kufanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa watuhumiwa wakuu wanaoendesha mtandao wa maharamia wanaoteka meli kwenye pwani ya bahari ya Hindi.Polisi mjini Mogadishu wamethibitisha kukamatwa kwa Mohamed Garfanji siku ya Jumapili jioni akiwa na walinzi wake wenye silaha ambapo polisi walipokea taarifa toka kwa wananchi kuhusu eneo aliko kiongozi huyo.
Mohamed Garfanji ni miongoni mwa watuhumiwa wakuu wa uharamia ambao wamehusika na matukio ya utekaji meli kubwa za kigeni zinazopita kwenye eneo la pwani ya Somalia na kujipatia mamilioni ya fedha baada ya kulipwa na wamiliki wa meli hizo ili kuziachia.Mwaka jana rais Hassan Sheikh Mohamud alitangaza kutoa msamaha kwa maharamia wadogo kujisalimisha na kuacha shughuli zao, hatua aliyochukua kujaribu kumaliza uharamia kwenye bahari yake lakini akasema msamaha huo hautawahusu viongozi wao.
Marekani na Sychelles zinataka kumuhoji mtuhumiwa huyo kwa madai ya kuhusika kwenye utekaji wa raia wake
No comments:
Post a Comment