Hii ndiyo
Barua aliyoandika Mtangazaji mahiri wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi
Baraka Kitenge akiacha kazi Redio One Stereo.
|
Mtangazaji
mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akisaini Mkataba wa kazi na
kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam.Kushoto
ni Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela.
|
Mtangazaji
mahiri wa habari za michezo,Maulidi Baraka Kitenge akipeana mikono
na Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela wakati wa
kubadilishana mikataba baada ya kusainishana jioni hii katika makao makuu ya
Radio hiyo,yaliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
|
Mtangazaji mahiri
wa habari za michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge
amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7
kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam leo.
Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.
Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa
vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwake kwa mtangazaji
huyo kinara kuhamia katika kituo hicho.
“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.
“Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni katika kipindi cha michezo hapa EFM”, alisema mkuregenzi huyo.
Maulidi Kitenge au
jezi nambari tisa mgongoni, amejiunga na magwiji walio bobea katika fani hiyo
akiwemo Dizo one,Dennis Sebo,Sos B,Kanky Mwaigomole na Dj Majay.
No comments:
Post a Comment