Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Luteni Msaafu Chiku Galawa
|
Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKOA wa Tanga umetenga vituo kadhaa
vya afya vitatu, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kudhibiti watu watakaobainika
kuambukizwa virusi vya homa ya ebola
Vituo hivyo ni cha kwenye mpaka wa
Horohoro wilayani Mkinga, Masiwani Shamba na Maramba. Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Chiku Gallawa alibainisha hayo juzi katika mkutano na waandishi wa habari.
Alisema timu maalumu ya mkoa ya
wataalamu wa afya, tayari inakagua uwezo wa vituo vingine vilivyotengwa na
halmashauri nyingine za mkoa huo, kama vinastahili kupokea wagonjwa wa aina
hiyo.
Alisema ingawa mpaka sasa hakuna
mgonjwa wa ebola nchini, serikali imechukua hadhari hiyo, kuwaondoa wasiwasi
wananchi kutokana na mwingiliano wa wageni kutoka nchi jirani kupitia mpaka wa
Horohoro.
Alisema vituo hivyo vitatu
vimeimarishwa kwa kupelekewa vifaa tiba, madaktari na wauguzi wenye stadi za
kutosha na vitatumika kutoa huduma kwa wagonjwa watakaobainika.
“Kwa kuwa ebola haina chanjo wala
tiba, mpango mkakati wa mkoa sasa ni kuhakikisha wananchi wanaelimishwa kuhusu
namna ya kujikinga kuzuia maambikizi…pia tumeziagiza halmashauri zote 11
zinazounda mkoa kutenga maeneo sahihi ya kupokelea wagonjwa hao”, alisema.
Aliongeza, “wananchi ondoeni
wasiwasi na tunawataka muimarishe usafi wa mazingira, hakikisheni mnanawa
vizuri mikono kwa maji safi na sabuni…acheni kusalimia kwa kushikana mikono na
watu kila mahali”, alisema.
No comments:
Post a Comment