
Na Masanja Mabula.Pemba
Waumini wa dini ya Kikristo wametakiwa kushikanama pamoja
katika kuitetea Imani yao na kumtegemea Mungu iku zote za maisha yao .
wito huo umetolewa na Padri Festo Ulasa wa kanisa katoliki Parokia
ya Wete wakati wa tafrija fupi ya kuumuaga iliyoandaliwa na waumini wa Jumuiya
ya Makangale na Kiuyu kwa Manda iliyofanyika kwenye kigango cha Makangale
juzi Padri Festo amesema kuwa ushirikiano wa waumini pamoja na sala zimekuwa ni
msaada katika utekelezaji wa majukumu yake ya kutoa huduma za kiroho Kisiwani
Pemba .
Naye Paroko ya Parokia hiyo Beatusi Babu aliyechukua nafasi
ya Festo amewataka waumini hao kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza vyema
majukumu ya kuwachunga kondoo wa bwana .
Aidha amesisitiza haja ya kuvichangia vyombo vinavyotumika kuenza
injili ikiwemo redio Maria ili kuwafikia wananchi kwa wakati mmoja .Akitoa
shukrani za waumini wa Jumuiya hiyo Katekista wa Kigango cha Makangale John
Simba Shija amemkuru padri Festo kwa huduma alizokuwa akitoa na kumtakia safari
njema na maisha meme katika kutoa huduma za kitume .
Padri Festo Ulasa ametakiwa kwenda kuendelea na kazi ya kutoa
huduma za kitume katika Nchi ya Uganda
No comments:
Post a Comment