
Na Msanja Mbula. Pemba
Jumla ya Miradi kumi na moja yenye thamani ya shilingi
milioni 305, 650,050 /= inatarajia kufunguliwa , kuzinduliwa na kuwekewa mawe
ya msingi na mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Kaskazini Pemba .
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini
Pemba Mhe Dadi Faki Dadi amesema kuwa miradi hiyo imeibuliwa na wananchi na
imelenga katika kuwapunguzi usumbufu katika upatikanaji wa huduma za kijamii .
Mkuu huyo wa Mkoa amefafanua kwamba ukiwa katika Wilaya ya Wete ,
Mwenge wa uhuru utatembelea miradi saba yenye thamani ya shilingi
milioni 226,490,050 .
Aidha ameeleza kwamba mwenge huo pia utazindua miradi minne yenye
thamani ya shilingi milioni 79,160,000 .Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi
kujitokeza kwa wingi wakati mwenge wa uhuru utakapokuwa unazindua ,
kufungua na kuwekea mawe ya msingi katika maeneo yao .
Mwenge wa uhuru unatarajia kuanza kukimbizwa katika Mkoa huo
tarehe 5 ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment