SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya
Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo
uliofanyika hivi karibuni.
TFF imesema uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanautambua, na wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.

“Tunapenda kuwakumbusha wanachama
wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao,
kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF
inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu,”.
“Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake,”.
“Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi,”imesema taarifa ya TFF.

No comments:
Post a Comment