
SHIRIKISHO la Soka la Ghana-GFA limetoa taarifa ya kuinyima ruhusa Sierra Leone ya kutumia moja ya viwanja vyake kwa ajili ya mechi yao ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika. Sierra Leone ilikuwa imeomba ruhusa kucheza baadhi ya mechi zake za kufuzu michuano hiyo nchini Ghana kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola nyumbani kwao

Katika taarifa ya Shirikisho la Soka
barani Afrika-CAF iliyotolewa jana imedai kuwa Sierra Leone walielekeza mechi
zao za nyumbani katika mzunguko wa mwisho wa kufuzu zichezewe Ghana. Baada
ya CAF kutuma maombi hayo ya Sierra Leone kwenda kwenye mamlaka husika Ghana,
GFA walijibu kwa kuwataka majirani zao hao kushughulikia suala hilo
kiserikali.
GFA limelitaka Shirikisho la Soka la
nchini hiyo kutuma maombi yao serikalini kwani suala hilo linahusisha mambo ya
afya hivyo wao watakuwa hawana kauli kwenye hilo.
No comments:
Post a Comment