
Halmashauri ya jiji la tanga imehaidi kuwapatia vijana
asilimia tano ya fedha kutoka vyanzo
vyake vya mapato ya ndani katika mwaka wa fedha 2014/2015 ili kutunisha mfuko
wao wa sacoss.
Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa jiji la tanga denisi misana wakati akiongea na vijana kwenye kilele cha
maadhimisho wa siku ya vijana duniani
yaliyo fanyika kiwilaya katika viwanja vya tangamano.
Hata hivyo katibu tawala wilaya ya tanga bernad patric amewakumbusha vijana wa jiji la tanga watumie
fursa ya elimu waliyonayo kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha
zikiwemo ukosefu wa ajira na uvutaji wa madawa ya kulevya.
Maadhimisho hayo ambayo yamefikia kilele chake 12agost
yaliambatana na midahalo na burudani mbali mbali ambazo zilibeba kauli mbiu
ikisema vijana na afya ya kili.
No comments:
Post a Comment