![]() |
|
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Msambweni Bi Halima Muya(Kushoto) na Mkurugenzi
wa KOICA nchini Tanzania Seung-Beom Kim(Kulia) wakizindua jengo la maabara ya Masomo
ya Sayansi shuleni hapo.
|
Na Evelyn Balozi. TANGA
SHIRIKA la maendeleo
la Korea Kusini KOICA limeipatia shule ya
sekondari Msambeni Mkoani hapa msaada wa vifaa vya shule vyenye thamani ya zaidi
ya shilingi mil 27 ili kusaidia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Akikabidhi msaada huo mkurugenzi wa
KOICA nchini Tanzania Seung-Beom Kim amesema ili kufikisha maendeleo kwa
wananchi serikali ya nchi yoyote duniani ni lazima kuwekeza katika elimu kama
ambavyo Korea Kusini imefanya na kuifanya kuwa taifa kubwa licha ya kutokuwa na
rasilimali yoyote katika ardhi yao.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya
mchepuo wa sayansi yenye miaka mitatu sasa, Halima Muya alisema watatumia
msaada huo kuwaandaa wanafunzi wanaopitia shuleni hapo ili kuandaa wasomi na
walimu wa masomo ya sayansi ambao ni hitaji kubwa kwa taifa.
Alisema nchi haita weza kukabiliana
na wimbi la upungufu wa wanasayansi hususani walimu kama hakutachukuliwa hatua
za makusudi kwa kuwaandaa tangu mashuleni.
Vifaa vilivyo tolewa ni Kompyuta
moja, Printa moja, Projekta moja, vitabu 720 kwa kila kidato kwenye kila somo
la sayansi kupewa vitabu 60 pamoja na uingizaji wa umeme kwenye shule hiyo.
![]() |
|
Mkurugenzi
wa KOICA nchini Tanzania Seung-Beom Kim (aliesimama) akizungumza wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano ya Misaada kwa Shule ya Sekondari Msambweni jijini
Tanga
|
Aidha KOICA imeboresha chumba cha
maabara kwa shule hiyo pamoja na kuwezesha vifaa ikiwemo kemikali za kufanyia
mazoezo ya vitendo, kabati la kuhifadhia vifaa vya maabara, viatu vya maabara,
meza tatu na viti 60.
Nae kaimu katibu tawala Mkoa wa
Tanga Monica Kinala alishukuru KOICA kwa kuendeleza juhudi za serikali nchini
kusogeza mbele elimu na kuwataka wasichoke kuwezesha wananchi elimu ya juu
pamoja na ufadhili wa masomo.
Akitoa shukrani kwa niaba wanafunzi,
mwenyekiti wa bodi ya wazazi na walezi Salimu Kisauji aliahidi msaada huo
kutumika kwa amanufaa ya wengi huku akiiomba KOICA waendelea kuwezesha walimu
zaidi wa masomo wa sayansi ambao idadi yao ni haba shuleni hapo.
Shirika la maendeleo ya Korea kusini
lina walimu wa kujitolewa 88 wanaofundisha nchini wakiwamo Eun Jung anaefundisha
sekondari ya Toledo, Sang Hoon Kim sekondari ya Galanosi, Seung Yoon Choi wa
Nguvumali, Jinwon OH wa Msambeni na Song Hyun Mi wa Masechu za jijini Tanga.


No comments:
Post a Comment