![]() |
|
Msemaji wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja akizungumza na wanahabari
(hawapo pichani) kuhusiana na habari iliyochapishwa na gazeti la Majira
toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa cha
habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=”. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Frank Mvungi. (Picha na Maktaba).
|
Serikali imetenga fedha zitagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri
nasaha na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 vilivyo chini ya
Idara ya Ustawi wa jamii nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la
Majira toleo Na. 7524 Vol.II/5624 la Jumatano Agosti 13, mwaka huu yenye kichwa
cha habari “Mahabusu ya watoto yadaiwa mil. 1/=
Mwamwaja alisisitiza kuwa deni hilo litalipwa kweye mahabusi hiyo iliyoko
Tanga.
Mahabusu hiyo ni miongoni mwa vituo kadhaa vilivyo chini ya Idara ya
Ustawi wa Jamii ndani ya Wizara ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Matumizi ya fedha hizo ni pamoja na kushughulikia tatizo la maji na uhaba
wa chakula kituoni hapo ili kuendelea kutoa huduma stahiki kwa watoto hao na
kufikia lengo la kuwarekebisha tabia zao ili wawe raia wema nchini.
Aidha, Mwamwaja aliongeza kuwa fedha zilizotengwa si za Mkoa wa
Tanga tu bali ni kwa ajili ya vituo vya nchi nzima zikiwemo makambi ya wazee
wasiojiweza, mahabusi za watoto na kambi za kutibu wagonjwa wa ukoma.

No comments:
Post a Comment