![]() |
WEZI HAO
WAKIHAMISHA FEDHA
|
Wanaume
wanane waliokua wamevalia mavazi maalumu meupe na vikaragosi usoni wakiwa na
mitutu mkononi walilizuia gari iliyokua ikisafirisha kiasi kikubwa cha pesa
mapema wiki hii kikadiriwa kua ni dola milioni kumi za kimarekani sawa na
paundi sita nukta mbili za Uingereza. wizi huo umeelezwa kua ni wa kihistoria
katika uhai wa taifa la Chile.
Mashuhuda wanasema kuwa pesa hizo zilikua njiani kupakiwa ndegeni na kupelekwa katika Bank za nchi hiyo na katika machimbo ya madini huko Copiapo,kaskazini mwa Chile.mkanda wa video uliopatikana na polisi dakika mbili baada ya tukio unaonesha genge hilo likiwasili ndani ya mavazi meupe na kujitia ni wamoja kati ya wafanyakazi katika gari hilo ingawa kamera za mahali hapo hazikunasa tukio hilo likitekelezwa.
Waziri wa mambo ya ndani wa Chile Mahmud Aleuy amesema kua polisi katika uwanja huo wa ndege walichanganyikiwa baada ya kuzidiwa maarifa na majambazi hao waliokuwa wamejipanga sawasawa kutekeleza tukio hilo na kusema kua polisi walipaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu wakati fedha hizo zikisafirishwa , na kwamba kazi ya usafirishaji wa vifurushi na mizigo zilikua ni za mamlaka ya anga na sio polisi.
Baada ya kufanikiwa kupora kiasi hicho cha pesa! Majambazi hayo yalijigawa katika makundi mawili tofauti na kuondoka kila moja na njia yake na kusambaza misumari nyuma yake na baadaye gari moja ilitelekezwa na kukutwa tupu jirani na eneo la tukio .
No comments:
Post a Comment