![]() |
| Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Michael Lucas Chikoma akikabidhi misaada katika kituo hicho mbele ya Wanajumuiya wenzake. |
![]() |
| Picha ya Pamoja ya Wanajumuiya na Watoto wa kituo hicho kuonesha Upendo na Mshikamano. |
![]() |
| Wanajumuiya Mama Toni( kushoto) na Mama Biata(kulia) walionesha mfano mzuri wa Mama mpenda watoto kwa kuwapakata watoto wadogo wa kituo hicho. |

![]() |
| Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Michael Lucas Chikoma akiwa amembeba Mtoto aliyeokotwa chooni Pongwe mwezi mmoja uliopita akiwa ametupwa na Mama yake baada ya kuzaliwa, Mtoto huyu analelewa katika kituo hiki akiwa na Afya njema. |
![]() |
|
Mwanahabari wetu Rebeca Duwe akifanya
mahojiano na Sister
Consolata Aloyce |
![]() |
|
Wanajumuiya
Asack na Geofrey wakishusha misaada kutoka kwenye gari.
|
Na Rebeca Duwe. TANGA
JAMII imeombwa kuwasaidia watu wenye mahitaji na kuwa na bidii ya
kuwatembelea watoto yatima wanaoishi kweneye vituo mbalimbali hapa nchini ili
wapate Baraka kutoka kwa Mungu.
Haya
ameyasema Sister Consolata Aloyce wa kituo cha nyumba ya furaha kilichopo
maeneo ya Bombo (Casa Famigria Rosseta) jijini hapa wakati akiongea kwa niaba
ya mkurugezi wa kituo hicho Sofia Malera
mbele ya Wanajumuiya ya Moyo
Mtakatifu wa Yesu kutoka Kigango cha Mtakatifu Gerad Parokia ya Mtakatifu Petro
Saruji Pongwe walipowatembelea watoto wa kituo hicho.
Katika
hatua nyngine Sister amewataka wale wasichana ambao wanawatupa watoto kwa namna
moja ama nyingine waache tabia hiyo, kwani ni
laana katika matumbo yao na hata mbele
za Mungu na wanajitengenezea machinjio kwa kizazi kijacho ndani ya
familia yao.
Naye
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Michael Lucas
Chikoma amewaasa jamii kuwakaribu na watoto yatima kuliko kujijali wao
wenyewe, ili wapate kuwasaidia kwa kuwapa chochote ambacho kinaweza kikawatia
moyo katika maisha yao kwani wana uhitaji kama watoto wengine.
Hata
hivyo Chikoma amesma kuwa wale ambao
watapata nafasi ya kuwatembelea watoto hao wawe mabalozi kwa wengine kwa ajili
ya kuwahamasisha kuja kuwasaidia watoto
yatima walioko kwenye vituo mbalimbali.






No comments:
Post a Comment