Awali michuano hiyo ilikuwa ianze Agosti 24 mwaka huu, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limelazimika kuisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).
Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.
Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.
Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.
SERENGETI BOYS
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boyz) inacheza mechi
ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja
wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi
hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na
kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi.
Serengeti
Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika
dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye
uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
Wachezaji
wanaounda kikosi cha Serengeti Boyz ni Abdallah Shimba, Abdulrasul Bitebo,
Abutwalibu Mshery, Adolf Bitegeko, Ally Mabuyu, Ally Mnasi, Amin Noren, Athanas
Mdamu, Badru Othman, Baraka Baraka, Hatibu Munishi na Issa Athuman.
Wengine
ni Juma Yusuf, Kelvin Faru, Kelvin Kamalamo, Martin Luseke, Mashaka Ngajilo,
Mechata Mnata, Mohamed Abdallah, Mussa Vicent, Nazir Barugire, Omary Omary,
Omary Wayne, Prosper Mushi, Seif Seif na Yahya Hafidh.
NIGERIA YAPIGWA STOP NA FIFA
NIGERIA
imesimamishwa na FIFA baada ya Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF, kuingiliwa
shughuli zake.
Hii
Leo FIFA imetoa taarifa kwamba Kamati ya Dharura imeamua kuisimamisha Nigeria
mara moja baada Mahakama Kuu ya Jos, Plateau State, kusimamisha shughuli za NFF
na kumtaka Waziri wa Michezo wa Nigeria kumteua Mtu kuendesha shughuli za NFF.
FIFA
imesema maamuzi hayo ni kinyume na Kanuni ya 13, Aya ya 1 na Kanuni ya 17, Aya
ya 1 ya Sheria za FIFA ambazo zinataka Vyama vya Wanachama wake kuendeshwa huru
na kutoingiliwa na upande mwingine wowote.
Hapo
Julai 4, Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, aliiandikia Nigeria na kuipa hadi
Julai 8 kuirudisha Madarakani NFF na kutoingiliwa tena kwa namna yeyote.
Barua
ya Valcke iliikumbusha Nigeria wajibu wake wa kuiruhusu NFF kuendesha shughuli
zake bila kuingiliwa na Mtu yeyote kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya Sheria za
FIFA.
Pia
Barua hiyo iliionya Nigeria kuwa endapo NFF haitarejeshwa madarakani ifikapo
Julai 8 basi Vyombo husika vya FIFA vitachukua hatua zaidi ikiwa pamoja na
kuisimamisha Nchi hiyo kwenye shughuli zote za Kimataifa za Soka ikimaanisha
kufungiwa kwa Timu yao ya Taifa na Klabu zao zote kucheza michuano ya Kimataifa.
Uamuzi
huu wa Leo utaifaya Nigeria isiweze kushiriki Mashindano yeyote ya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment