HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 4 July 2014

KIJANA AWASHAMBULIA WAZAZI KWA PANGA KISA KANYIMWA DAKU




Jeshi la polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia kijana Suleiman Gharib Amour ( 22) mkaazi wa Tumbe Wilaya ya Micheweni anayedaiwa kuwashambilia kwa mapanga wazazi baada ya kunyimwa daku.

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa huo Shakhan Mohammed Shekhan ambapo amewataja waliojeruhiwa kwenye tukio hilo kuwa ni Gharib Amour Khamis (60) na Mariam Amour Khamis 935) wote ni wakazi wa Tumbe .

Kamanda Shekhan amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia alihamis majira ya saa tisa za usiku baada ya wazazi hao kugoma kumpa daku mtoto wao kutokana na kile walichodai kwamba alikuwa amelewa pombe .

Aidha kamanda Shekhan ameeleza kwamba majeruhi wa tukio hilo wamelazwa kataika hospitali ya Micheweni wakipatiwa matibabu na wamejeruhiwa sehemu za mabegani , Mikononi pamoja na kichwani .

Kufuatia kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoa huo amewataka vijana kujiepusha na vitendo vya utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na kuheshimu maagizo ya wazazi wao .

Baadhi ya wananchi walioshughudia tukio hilo wamekiri kuwa kijana huyo alikuwa amelewa chakari na kitendo cha kunyimwa daku ni haki yake kutokana na kwamba huu ni mwezi ya toba .

Mwandishi wa habari ametembelea katika Hospitali ya Micheweni ambapo wanafamilia hao wamelazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kushughudia afya zao zinaendelea vyema.

No comments:

Post a Comment