KESI ya
shambulio iliyojeruhi na kusababisha upotevu wa zaidi ya sh milion
7.8 inayomkabili Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Chuo cha
Anga kilichopo Kange jijini Tanga, Meja Lemicho Msafiri, imeahirishwa.
Iliahirishwa mapema
jana katika Mahakama Kuu Mkoa wa Tanga na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Ramla
Shehagilo na kusema itaendelea Julai 28, mwaka huu.
Shambulio hilo
lilifanyika dhidi ya mstaafu mwingine wa jeshi hilo ambaye kwa sasa ni balozi
wa mtaa wa TRA/Jeshini, Nasibu Abdallah aliyevamiwa nyumbani kwake kisha
kupigwa, kujeruhiwa na kuharibiwa thamani za nyumbani kwake Desemba 20, 2012.
Imeelezwa kuwa meja
huyo alipewa taarifa kwa njia ya simu na mkewe akiwa nchini China kikazi na
kujulishwa kwamba balozi huyo alikwenda
nyumbani kwake na kumtukana kitendo ambacho mlalamikaji amedai si kweli. Hata hivyo mshitakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.
nyumbani kwake na kumtukana kitendo ambacho mlalamikaji amedai si kweli. Hata hivyo mshitakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment