MSHAMBULIAJI Betram Mombeki amejiunga na JKT
Ruvu Stars ya Pwani- maana yake ameijiondoa Simba SC.
Pamoja na kuonyesha uwezo wa kuridhisha akiwa Simba SC msimu uliopita, lakini Mombeki alijikuta katika wakati mgumu mbele ya kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Pamoja na kuonyesha uwezo wa kuridhisha akiwa Simba SC msimu uliopita, lakini Mombeki alijikuta katika wakati mgumu mbele ya kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Loga alikuwa akimuacha benchi Mombeki, na hata alipoamua kumuingiza, wakati mwingine alimtoa katika mechi baada ya kufanya kosa kidogo, jambo ambalo wazi limemkera mshambuliaji huyo mwenye nguvu na ameamua kwenda kujaribu maisha mapya.
Mombeki ndani ya Uzi wa JKT Ruvu Stars |
Mombeki
mwenyewe hakutaka kuzungumza mengi zaidi ya kusema; “Ndiyo, nipo hapa sasa,
naangalia ustaarabu mpya,”.
Meneja wa JKT Ruvu Stars, Suleiman Oga amesema wamempokea Mombeki na wapo katika mazungumzo naye kwa ajili ya kumsajili.
Kocha Freddy Felix Minziro leo amempanga Mombeki JKT Ruvu ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Dimbani dhidi ya Azam |
No comments:
Post a Comment