Viongozi na wanachama wa Chama cha Vijana Wakatoliki wa Group ya Facebook walipotembelea na kutoa misaada katika kituo cha kulelea watoto yatima Raskazone Jijini Tanga(Picha na Maktaba) |
Jamii nchini kote
wametakiwa kuwa na desturi ya kupenda kuwatembelea watoto yatima na walemavu
wakila namna wakiwemo waleamavu wa ngozi, ,wasioona au wenye uoni hafifu pamoja
na walemavu wa viungo.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hii ofisini kwake mch.kiongozi wa kanisa la kiinjili la
kilutheri Tanzania KKKT Usharika Makorora jijini JOHN NDIMBO hapa amesema kuwa
jamii isahau kuwa kuwatembelea vituo vya watoto yatima na walemnavu kwani ni
jukumu la kila mtu kuona umuhimu wa kuwatunza watu kama hao ili wapate kuishi
kama watu wengine.
Aidha amesema kuwa
katika kuwa saidia watu kama hao nchi inaweza kupata baraka kutoka kwa mungu
lakini pia ni agizo la Mungu kwa wanadamu hususani wale wenye imani ya
kumwamini Mungu kama ambavyo neno linasema dini ilyosafi ni ile inayokwenda
kuwatazama yatima na wajane.
Katika hatua nyingine
amesema kuwa wale ambao wanatabia ya kuwanyanyasa watoto kwa namna moja ama
nyigine wanapaswa kuacha haraka iwezakaavyo kwani dhambi mbele za Mungu kwani
klia aliyeumbwa na Mungu anapaswa kuishi.
Sambamba na hayo
amesema kuwa jamii ione umuhimu wa kutoa fadha na mali walizo nazo kwaajili
watoto wenyemahitaji ya kila namna ikiwa ni pamoja na kupelekwa shule na kupewa
elimu ihuyo stadi za maisha.
Naye
Mshagulwa Ruben ambaye ni mratibu wa kituo cha watoto wasiona( blinde
school)kilichopo Irente wilayani Lushuto amesema kuwa watanzania wana jukumu la
kuona mahitaji ya watoto hao kwani changamoto nyingi ni ukosefu wa fedha
za kuendesha maisha yao kwani baadhi yao wanakaa mbali na maeneo ya shule hivyo
ameomba jamii iangalie suala hilo kwa jicho la ndani.
No comments:
Post a Comment