Kutokana na ongezeko la wagonjwa katika Kituo cha Afya Pongwe mahitaji mbalimbali yanahitajika ili kuboresha huduma ya Afya kituoni hapo.
Akizungumza mbele ya kamati ya Uchumi,Elimu, na Afya ya halmashauri ya jiji la Tanga iliyofanya ziara yake katika kituo hicho, mmoja wa Madaktari aliyejitambulisha kwa jina la Dkt. Feisal, amesema kuwa shughuli za tiba katika kituo hicho zinakwenda vizuri isipokuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiutendaji.
Amezitaja changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na
ukosefu wa gari la wagonjwa,upungufu wa vifaa tiba, na kukosekana umeme wa
uhakika hali ya kuwa huduma za operesheni hufanyika kituoni hapo.
Aidha Dkt. Feisal ameiomba kamati hiyo ya halmashauri kuwapatia jenereta ili liweze kusaidia katika huduma za upasuaji pamoja na gari la wagonjwa litakalorahisisha wananchi kupata huduma kwa wakati.
Mwisho ameiomba halmashauri kuongeza gharama za uchangiaji wa huduma za upasuaji ili ziweze kukidhi mahitaji ya vifaa tiba kutokana na vifaa vya huduma hiyo kuwa na gharama kubwa.

No comments:
Post a Comment