Inaarifiwa
kuwa Wapalestina kama 50 wameuwawa katika mtaa mmoja wa Gaza katika shambulio
kubwa kabisa la mizinga tangu Israil kuanza mashambulio yake.
Makubaliano ya
kusitisha mapigano baina ya Israil na Hamas huko Shejaiya ili kuruhusu magari
ya wagonjwa kuingia huko, yalidumu saa moja tu, na yameanza tena.
Mwandishi wa
BBC ambaye ametoka Shejaiya hivi punde, anasema kabla ya mapigano kusita kwa
muda mfupi, mizinga ya Israil ikifyatuliwa mfululizo na hivo kufanya jamii yote
kukimbia.
Anasema nyumba
nyingi sasa zimebaki kifusi tu.
Wakuu wa
Palestina wanasema watu zaidi ya 400 wameuwawa Gaza katika siku 13.
Waisraili saba
wamekufa, wakiwemo raia wawili.
Ripoti kutoka
Qatar zinaonesha kutafanywa mkutano huko Jumapili baina ya Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Ban Ki Moon, na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, katika juhudi za
kutafuta makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano huko Gaza.
Qatar imekuwa
kama mjumbe wa Hamas.
Kiongozi wa
Hamas ambaye yuko uhamishoni, Khaled Meshaal, anaishi katika nchi hiyo ya
Ghuba.
Wakuu wa huko
wanasema wamepokea orodha kutoka Hamas ya shuruti zake kabla ya mapigano
kusitishwa.
:CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment