Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Mhingo
Rweyemamu
(Picha na Maktaba)
|
Na Godwin Lyakurwa (Tanga News)
KIASI nyumba kumi za wananchi wa kata ya
kwamatupu tarafa ya Sindeni wilaya ya Handeni mkoani hapa zimechomwa moto jana
na watu wanaodhaniwa kuwa mgambo wakiongozwa na diwani wa tarafa hiyo Mustapha
Bereko.
Akizungumza na Mtandao huu shuhuda wa
tukio hilo Mch Obedi Moleli amesema kuwa diwani huyo amefikia hatua hiyo ya
kuchoma moto kwa madai ya kuwatuhumu raia hao ambao ni wakulima na wafugaji kuwa
wamevamia eneo hilo aliloliita hifadhi ya misitu wa kata.
Wakazi hao waliamia kijijini hapo zaidi ya miaka
minne iliyopita kutokea Mkoani Arusha na waliuziwa maeneo hayo na wenyeji
ambaponyumba zao hazikuguswa na eneo hilo.
Hata hivyo wananchi wa eneo hilo wamedai
kuwa mara baada ya kuwasiliana na Jeshi la Polisi hawakuweza kupewa ushirikiano
wowote kwa madai kuwa diwani huyo Bereko anafahamiana na vigogo wa jeshi hilo
Alipotafutwa na radio huruma kuthibitisha
madai hao Afisa upelelezi wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Tanga RCO Kimata Aziz alionyesha kushangazwa na taarifa na
kuomba atafutwe baada ya muda kwakuwa hakuwa akizifahamu taarifa hizo ingawa alipotafutwa
alipokea simu bila kuzungumza lolote kisha akaizima.
No comments:
Post a Comment