Baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga wameipongeza halmashauri ya jiji hilo
kwa hatua walioichukua ya kuweka matuta katika barabara nyingi za jiji za jiji la Tanga
Hatua hiyo imeonekana kuwa muhimu kwa kile kinachotajwa kuwa ni sehemu ya kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea kwa wingi katika barabara nyingi hususan zilizopo katika kiwango cha lami.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa Kwakaheza jijini hapa Ustadh Juma Abdallah Ngeda na Zubeir Yusuf Kilua wamesema kuwa hatua hiyo itapunguza kasi ya ajali za barabarani kwani kabla ya kuwekwa matuta hayo wamekuwa wakishuhudia ajali nyingi zinazotokana na mwendokasi wa vyombo vya moto.
Aidha Ustadh Juma ameshauri watumiaji wa barabara wakiwemo wenye vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu, kuzingatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.
No comments:
Post a Comment