HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 20 July 2014

AFCON 2015: STARS, MSUMBIJI 2-2, MATUMAINI SASA NI FINYU..!!


KIKOSI CHA TAIFA STARS

TAIFA STARS Leo wamejiweka pagumu kufuzu kuingia Hatua ya Makundi ya kusaka nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huko Morocco Mwakani, baada kutoka Sare 2-2 na Msumbiji kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Stars, wakiwa chini ya Kocha Mart Nooij ambae kati ya Mwaka 2007 na 2011 alikuwa Kocha wa Msumbiji, walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Penati iliyopigwa na Domingues lakini walijitutumua na kusawazisha kwa Bao la Mcha Khamis ambae pia alifunga Bao la Pili kwa Penati.
Hata hivyo, kazi hiyo njema ilipotea bure baada ya kuwaruhusu Msumbiji kusawazisha katika Dakika ya 89 kwa Bao la Isaac Carvalho.
+++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Tanzania 2
-Mcha Khamis Dakika ya 66 & 71 [Penati]
Mozambique 2
-Gaspar Domingues Dakika ya 48 [Penati]
-Isac Carvalho 89
+++++++++++++++++++++++++++
Kwenye Marudiano huko Maputo, Msumbiji, Tanzania wanahitaji ushindi au Sare ya Bao 3-3 na kuendelea.
Kwenye Mechi nyingine iliyochezwa Leo huko Setsoto Stadium, Maseru, Wenyeji Lesotho waliifunga Kenya Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 70 la Moletsane.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19
Uganda 2 Equatorial Guinea 0
Botswana 2 Guinea-Bissau 0
Sierra Leone 2 Seychelles 0
Jumapili Julai 20
Lesotho 1 Kenya 0
Tanzania 2 Mozambique 2
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
** Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau

No comments:

Post a Comment