Shughuli
ziliathirika leo wilayani Mityana baada ya ndege kutua kwa dharura katika
barabara ya magari ya Mityana.
Ndege
hiyo N604AR, iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Marekani, ilitua katika eneo la
Kiwawu umbali wa kilomita 22 kutoka wilaya ya Mityana.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Nation, kamishna wa wilaya Joel Walusimbi, alithibitisha
tukio hilo akisema rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua katikati ya barabara
Polisi
walisema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea mjini Juba Sudan Kusini kutoka
uwanja wa ndege wa Entebbe.
:KUTOKA BBC
No comments:
Post a Comment