Mkuu wa wilya ya Tanga Halima Dendego |
Shule ya msingi
Pongwe yenye wanafunzi mahitaji maalum iliyopo jijini Tanga inahitaji kiasi cha
sh.milioni 240 kwa ajili ya ujenzi wa uzio shuleni hapo pamoja na ununuzi wa
vifaa vya kufundishia.
Hayo yalisemwa na
mwalimu mkuu wa shle hiyo, Yahaya Mafita,wakati akipokea msaada wa
vitanda vyenye thamani ya sh.milioni 1.2 kutoka chama cha kuweka na kuweka
(Saccos) cha Tanga cement.
Alisema shule hiyo
inauhaba mkubwa wa vifaa vya kufundishia, huku wanafunzi 32 wakihitaji mashine
za nukta nundu lakini zinazofanya kazi ni saba pekee.
Alisema kuwa shule
hiyo ina madarasa kumi pekeeambayo yanatumika kufundishia wanafunzi 90 kwa
wakati mmoja, huku kati yao wenye mahitaji maalum wakiwa watano.
Tunaomba wasamaria
wema na serikali watusaidie kwani shule yetu inachangamoto kubwa ya vifaa vya
kufundishia pamoja na mabweni ya kisasa ya kulalia wanafunzi wenye mahitaji
maalum “Alisema Mafita.
Aidha, alisema
ukosefu wa mitaala maalum kwa watu wenye uono kwani inalazimu shule kuingia
gharama ya kudurusu upya kwa kukuza maandishi ya vitabu vya mitaala ili waweze
kusoma vizuri.
Mwenyekiti wa
Saccos ya Tanga cement, Endrew Pesa, alisema msaada huo unatokana na faida
waliyoipata kwenye Saccos hiyo ambayo wanaitumia kusaidi makundi maalum yenye
mahitaji kama wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo.
Alisema wametoa
vitanda 10 pamoja na mgodoro yake kama sehemu ya ahadi waliyoitoa kwa mkuu wa
wilya ya Tanga Halima Dendego ili kupinguza uhaba wa vitanda katika shule hiyo.
No comments:
Post a Comment