Gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa shindano Nice & Lovely Miss Tanga 2014 |
Gari ambalo atakabidhiwa mshindi wa shindano kubwa
nala kipekee linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa mkoa wa Tanga, Nice &
Lovely Miss Tanga 2014 tayari limepelekwa mkoani humo na sasa lipo katika
maegesho ya magari katika hotel ya Mkonge.
Mkurugenzi wa kampuni ya Mac D Promotion ambao ndio
waandaaji wa shindano hilo, Irene Rweyunga amesema mwaka huu
wampaniakuhakikisha wanapata washiriki wenye sifa na viwango lengo likiwa ni
kuhakikisha mshindi anakuja kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mwaka
huu.
Irene amesema mwish wa kuchukua na kurudisha fomu za
kuhiriki shindano hilo ni jumampili hii ya tarehe 08 June 2014, na kambi rasmi
itaanza jumatatu ya tarehe 09 June 2014 katika hotel ya Tanga Beach Resort.
Shindano la Nice & Lovely Miss Tanga litafanyika
June 21′ 2014 katika Hotel ya Mkonge.
No comments:
Post a Comment