Picha zilizopigwa baada ya tukio |
Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la
kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu
ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez
pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na
kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Kutokana
na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe
la dunia.
Kutokana
na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa
hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe
28.
Adhabu
hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe
la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa
mashindano ya kombe la dunia.
Kamati
hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote
Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.
Mwenyekiti
wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu
tabia duni kama hii uwanjani hasa wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya
mashabiki kote duniani wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia
maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha
mchezaji huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''
Mashabiki
wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia
kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.
Lakini
mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay na shirikisho la kandanda nchini humo
wamemtetea mchezaji wao,wakisema hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye
huichezea Liverpool ya England
No comments:
Post a Comment