Uingereza inakabiliwa na
upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya
uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.Onyo hili limetolewa na shirika la
kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo
hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo
Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya
matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.Amesema
kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha
iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa kuwa upungufu huo
unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo
sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi
walipendelea kuficha majina yao.Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi
kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi
kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu
za kiume bado upo.Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu
zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya
kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila
mbegu kumi mnamo mwaka 2005.
No comments:
Post a Comment