MFANYABISHARA mmoja mkazi wa Michungwani wilaya ya Muheza
mkoani Tanga, Ally Rajabu Makufya 72, amejiua kwa kujipiga risasi ya shingo kwa
kutumia bunduki.
Marehemu ambaye pia ni mmiliki wa baa mbili wilayani Muheza
amejiua June 8 majira ya saa 3; 30 asubuhi akiwa chumbani kwake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe amesema kuwa Marehemu alitumia
Bunduki yake anayokuwa akiimiliki kihalali.
Kamanda Massawe amesema Jeshi la Polisi mkoani hapa bado
linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Wakati huohuo June 08 majira ya saa 8:20 mchana watu
wa wawili Jofrey Daniel (20) mkazi wa kwanjeka na Musa Hamisi miaka 44 mkazi wa
Mtambwe Mkoani hapa wamekamatwa wakiwa na bunduki Raifo yenye namba 2703520
iliyowahi kuripotiwa na Musa Hamisi 44 kwamba imeibiwa.
Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamekamatwa maeneo
ya Ngomeni barabra kuu ya Muheza -Tanga pia wakiwa na risasi mbili za bunduki
hiyo, ganda moja la risasi, panga moja, kisukimoja na bisi bisi mbili.
No comments:
Post a Comment