Hivi ndivyo choo ninavyoonekana kwa nje |
Hapa ni
ndani ya choo hicho,mazingira hatari |
Hili ndio
tundu la choo hicho ambapo mototo huyo alitupwa ndani na mzazi wake. |
Nguo alizokutwa
nazo mototo huyo zikiwa zimeanikwa baada ya kufuliwa na awasamaria wema
waliomtoa chooni.(anayeonekana katikati amekaa ni balozi wa mtaa huo Mr Mbogo) |
Hawa ni wakaazi
wa nyumba ambayo choo chake alitupwa mtoto huyo ,hapa wanazungumza na waandishi
wa mtandao huu waliofika kuchukua habari.(hawapo pichani) |
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
mwanamke mmoja anaesadikiwa kuwa mkaazi wa mji wa Pongwe jijini Tanga ambaye hakuweza
kutambulika amejifungua mototo na kumtupa chooni.
Tukio hilo la kinyama na la
kusikitisha limetokea usiku wa juni 12 ambapo watu wengi walikuwa makini kwenye
luninga zao kufuatilia mchezo wa kwanza wa michuano ya kombe la Dunia nchini
Brazil.
Hata hivyo jitihada zilifanywa na
majirani waliopo karibu na eneo la tukio kunusuru maisha ya mtoto huyo hii ni
kufuatiwa na mwanamke mmoja aliyekwenda msalani kujisaidia ambapo alisikia
sauti ya mtoto huyo wa siku moja ikitokea ndani ya tundu la chooni
Ndipo alipoamua kupiga mayowe na
kuamsha ndugu zake ili washuudie tukio hilo na hapo kuomba msaada wa kumtoa
mototo huyo
Sanjari na hayo hawakusita kuelezea
juu ya tukio na kusema kuwa mototo huyo amepelekwa hospitali kuu ya mkoa
iitwayo bombo hospital kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment