| PICHA ZA ENEO HILO LINALO JAA MAJI WAKATI WA MVUA |
| Hii ni Hatari sana |
Wakazi wa mji wa Pongwe jijini Tanga
wamombwa kuwa na subira na uvumulivu kutokana na
changamoto inayo wakabili ambayo ni kujaa kwa maji kipndi cha mvua kubwa kandokando ya barabara kuu ya kutoka
tanga mjini kwenda Segera hasa katika eneo la Soko la Zamani ambapo karavati lililokuwa likitumika kupitisha maji limezibwa na mkandarasi aliyekuwa akikarabati barabara hiyo.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa kutengeneza
na kuhifadhi barabara tanrodi Mkoani
tanga injinia ALFRED NDUMBARO akizungumza na waandishi wa habari kutoka radio
huruma amesema kuwa swala hilo wanalifanyia kazi na mara baada ya mwaka wa
fedha unao aanza mwezi wa saba ili kutoa
kero hiyo inayo wasumbua wakazi wa Pongwe.
Hata hivyo injinia NDUMBARO ametoa ushauri na kusema kuwa halmashauri
inapaswa kutengeneza mitaro ili kuboresha miundo mbinu ya barabara za mitaa ili
kuondokana na tatizo la kujaa kwa maji mitaani.
No comments:
Post a Comment