
WIZARA ya afya na ustawi wa
jamii, kupitia serikali Mkoani Tanga imekanusha madai ya yanayo enezwa wa
wananchi juu ya kuwepo wagonjwa wanaougua homa ya dengue mkoani hapa.
Akizungumzia uvumi wa kuenea kwa
ugonjwa huo Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Asha Mahita, amewaambia waandishi wa
habari kuwa may 12 walipokea mgonjwa aliyeonesha dalili za ugonjwa huo
hatahivyo baada ya kufanyika vipimo ikaonekana hana ugonjwa huo.
Mahita amesema kuwa hata baada ya
kufanyika mawasiliano katika wilaya zote za mkoa wa Tanga tarifa za kitabibu
zimethibitisha hakuna mgonjwa aliyedhaniwa kuugua Dengue
Hata hivyo Mganga mkuu amewataka
wananchi kutosita kuchunguza afya zao katika vituo vya afya pale inapoonekana
dalili za ugonjwa huo na kutilia mkazo umuhimu wa kuendelea kufanyIKa usafi wa
mazingira ili kuzuia uwezekano wa mbu wa Aedes anaeambukiza ugonjwa huo
kuzaliana.
No comments:
Post a Comment