![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Mhingo Rweyemamu (wa kwanza kushoto) akizungumza na Wakulima wakati wa ziara yake Wilayani humo |
WILAYA ya Handeni
mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali
kuu kwa msimu ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao
yakiwemo mahindi na ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya
Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara
yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo
kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo
ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya
wataalam.
Akiwa katika mashamba
ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni,
Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema
katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana
uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha.
Amesema pamoja na
kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa
baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na
faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani.
Bw. Rweyemamu
amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha
hasa mahindi na ufuta.
Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.
Na kwa upande wao
baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu
wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita.

No comments:
Post a Comment