
Wito umetolewa kwa jamii kuwa
ishirikiane na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU)ili kuweza
kubaini na kukomesha matukio ya utoaji na upokeaji rushwa mkoani Tanga .
Hayo
yamesemwa na mkuu wa dawati la elimu kwa uma Salome Swai wakati
akizungumza na radio huruma ofisini kwake mkoani hapa ambapo amesema kuwa
ilikutokomeza vitendo vya rushwa ni wajibu wa kila mtu kutoa taarifa endapo
kutakuwa na ushaidi wa kutoa na kupokea rushwa.
Aidha amezitaja kesi walizo nazo kwa
mkoa wa Tanga katika mwaka 2013 na 2014
kuwa jumla ya kesi 56 ikiwa 19 ni mpya
na zote zipo mahakamani hii inadhihirisha kuwa vitendo vya rushwa bado
vinaendelea.
Hata hivyo takukuru imejipanga katika
kubaini na kukuhakikisha wanadhibiti vitendo vyote vya utoaji na upokeaji wa
rushwa kwa yeyote atakaye bainika na tuhuma bila kujali umri wala cheo.
No comments:
Post a Comment