![]() |
| Bi Regina Gwae ( wapili kushoto), Akiongea na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and lovely jijini Dar es Salaam kuhusu shindano la miss Tanga linalotarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge hotel (watatu kulia),Meneja Mauzo Nice and lovely Bw.Brian Kelly. |
![]() |
| Bi Regina Gwae (kushoto),akiwaonyesha waandishi wa habari gari lenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Nice and lovely litakaloshindaniwa katika shindano hilo (kulia), meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw.Brian Kelly. |
Wito umetolewa kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza
kwa wingi kushuhudia shindano kubwa na la aina yake la kuwania taji la
urimbwende linalotarajiwa kufanyika tarehe 21 juni 2014 katika ukumbi wa Mkonge
hotel.
Akiongea na wana habari kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Nice and
lovely Bi Rejina Gwae amesema kuwa wanajivunia kupata nafasi ya kuwa waandaji
wa shindano hilo na kutoa wito kwa warembo wote wenye nia ya kushiriki
kujitokeza kwa wingi.
Kuhusu zawadi kwa mshindi Bi Rejina amesema kuwa mshindi ataondoka na
gari lenye thamani ya shilingi miliono 10 toka kwa kampuni ya Nice and lovely
akasema kuwa pia kuna zawadi nyingine za pesa taslimu toka kwa washindi wengine
ambazo wanatarajia kuzitangaza baadae.
Kwa upande wake meneja mauzo wa Loreal wamiliki wa bidhaa za
Nice and lovely Briyan Kelly alianza kwa kuishukuru kampuni ya Mac D promotion
kwa kuwapa nafasi ya kuwa wadhamini wa nafasi hiyo na kuahidi kuitendea haki
nafasi hiyo.
Akamalizia kwa kutoa wito kwa wote wenye nia ya kushiriki katika shindano
hilo kujitokeza kwa wingi na kusema kuwa fomu za kushiriki zinapatikana Mkonge
hotel, D,boutique tanga mjini,Breez fm,Tanga beach resort, Five brothers,
Mwambao fm, Sophia records, Danny fashion barabara ya 13, ofisi za the guardian
tanga barabara ya 15 na Yolanda salon mtaa wa Eckenford na Nyumbani
hotel.


No comments:
Post a Comment