
MWANASHERIA Damas Ndumbaro amepewa jukumu la kuongoza kamati ya uchaguzi wa Simba sc kwa lengo la kupata warithi wa viongozi wasasa wanaoongozwa na mwenyekiti, Ismail Aden Rage.
Kamati ya uchaguzi imeanza kazi hiyo baada ya serikali kukabidhi katiba iliyofanyiwa marekebisho kwa uongozi wa Simba sc.
Uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini mapungufu katika vipengele kadhaa katika katiba yao yalikwamisha .
Lakini jana katibu mkuu wa Simba sc, Ezekiel Kamwaga alitangaza kuwa tayari serikali imemaliza zoezi lake na kukabidhi katiba.
Kwa misingi hiyo, Kamati ya uchaguzi haina cha kupoteza zaidi ya kuanzisha rasmi mchakato mzima wa kupata viongozi wapya wa klabu.
Tangu Rage aingie madarakani miaka miwili iliyopita kumekuwepo na changamoto nyingi na mivutano isiyoisha.
Si rahisi kujua kama Rage alikuwa mbaya katika uongozi wake kwasababu inasemekana kuna watu wachache walikuwa hawampendi ndani ya uongozi na kupandikiza chuki kwa wanachama ili aonekane hafai.
Majaribio kadhaa ya kutaka kumpindua Rage yameshuhudiwa bila mafanikio
Katiba ya Simba imekuwa ikimlinda kwa wakati wote, hivyo wale wanaojaribu kumpindua kugonga mwamba.
Unakumbuka sakata la aliyekuwa kaimu mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang`are `Mzee Kinessi` na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.
Kinessi alitangaza kumsimamisha mwenyekiti Rage, lakini mwanaume huyo aliyekuwepo nje ya nchi alirudi na kuita kikao chao kama kikao cha harusi na yeye atabaki kuwa mwenyekiti.
Hata TFF walitangaza kumtambua na akaendelea na majukumu yake klabuni.
Pia wanachama wa baadhi ya matawi walishakutana mara kadhaa kutaka kumpindua Rage, lakini waliishia kuzodolewa na mkuu wao huyo.
Rage aliweza kuyafanya hayo kwa misingi ya katiba ya Simba waliyoiandika wanachama wenyewe.
Wakati Rage anaingia madarakani, alikuja na mipango mizuri ili kuiweka Simba klabu ya kisasa.
No comments:
Post a Comment