| Bango la Jiji la Tanga lenye Ujumbe wa Usafi |
| Uchafu ukiwa umezagaa kwenye soko maarufu la Mgandini jijini humo |
WAFANYA biashara wa mazoa
ya nafaka na samaki waliopo barabara ya 15 Kata ya Ngamiani Kusini mijni hapa,
wameiomba Halmashauri ya jiji la Tanga kusimamia usafi wa mifereji iliyopo
kandokando ya barabara hiyo ambayo imekuwa
chanzo kikuu cha kuwepo kwa magonjwa ya milipuko pamoja mazalia ya mbu hususani kipindi cha mvua.
Wakizungumza
na Redio huruma kwa nyakati tofauti Akida Ramadhani na Kimaro Gilioni wamesema
wao wamekerwa na hali ya uchafu uliopo ndani ya mifereji hiyo ambayo inasababisha maji machafu kutuama
jambo amablo linahatirisha afya wakazi
wa eneo hilo.
Wafanya
biashara hao wameiomba Halmashuri kuchua hatua
ya kusafisha mifereji hiyo ili maji yapite kwa uraisi badala ya wafanya biashara
kuhangaika wenyewe kuwatafuta vibarua na kuwalipa wenyewe kwa muda mrefu.
Akilizungumzia
suala hilo Mwenyekiti wa Mtaa wa Jamhuri
Kata ya Ngamiani Kusini, Shaban Choyo amesema kuwa ni wajibu wa kila mfanya buiashara kusimamia
usafi katika eneo hilo hali ambayo itasaidia
kuondokana na magonjwa ya mlipo kama Dengue na mengineyo.
Amesema
yeye kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kata watahamasisha jamii
zaidi juu ya usafi huo wa mifereji kama wanavyo fanya katika maeneo mengine
ikiwemo barabarani.
No comments:
Post a Comment