![]() |
| Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Baraka Kizuguto(Picha na Maktaba) |
Mkutano Mkuu wa Wanachama wa mabadiliko ya
baadhi ya Vipengele kwenye Katiba utafanyika siku ya jumapili Juni Mosi 2014
katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay kuanzia majira ya saa 3 kamili
asubuhi huku wanachama wote hai wa klabu ya Young Africans wakiombwa kujitokeza
kwa wingi.
Akiongea na waandshi wa habari makao makuu ya
klabu, Afisa Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema mkutano huo wa
siku ya jumapili ni kwa ajili ya marekebisho ya katiba kama maagizo ya
Shirikisho la Soka nchini TFF ilivyoagiza.
"Jumapili tunafanya makutano wa
marekebisho ya katiba lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata nafasi ya kutoa
maoni yao na kupitisha hivyo vipengele ambavyo vitapelekea Yanga kupeleka
katiba yake TFF na kisha kwa msajili ili shughuli zote za klabu ziweze
kufanyika kwa kufuata katiba mpya" alisema Kizuguto.
Mara baada ya mabadiliko hayo nadhani tutakua
tayari kuelekea kwenye mchakato wa Uchaguzi kwani tulikuwa tunasubiria
marekebisho ya Katiba tu, TFF na msajili wakishaiptisha Katiba basi tutakua
tayari kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi.
Watakoruhusiwa kuhudhuria mkutano mkuu siku
ya jumapili ni wanachama wa Yanga SC walio hai tu, kwa maana ambao wamelipia
ada zao za uanachama mpaka kufikia kwa mwezi ujao wa Juni 2014.
Wanachama ambao bado hawajalipia Ada zao za
uanchama wanaombwa kulipia mapema kabla ya siku ya mkutano, malipo yote
yanafayika kwenye Idara ya Fedha makao makuu ya klabu kila siku muda wa kazi na
siku ya jumamosi saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana.

No comments:
Post a Comment