
Hivi ndivyo Samaki wanavyosafishwa na kuandaliwa kabla ya kuuzwa kwa wateja katika Soko hilo maafufu jiji hapa(picha na Maktaba) |
BAADHI
ya wachuuzi na wanunuzi wa samaki katika mwambao wa bahari ya hindi eneo la
Chumbageni maarufu kama deep see mjini hupa wameilalamikia halmashauri ya jiji la
Tanga kwa madai ya kutowawekea mazingira masafi ya kufanyia biashara katika
maeneo hayo.
Wakizungumza
na mtandao huu kwa nyakati tofauti wanunuzi wa hao wamesema mazingira yaliyopo yamekuwa
tishio kubwa kwa afya zao kwa kuhofia kutokea magonjwa ya milipuko kama
kipindupindu hasa nyakati za mvua inakuwa vigumu kufika maeneo hayo.
Wamesema
kwa sababu ya barabara mbovu ya kuingilia baharini ambayo hujaa tope, wakati
mwengeni huteleza na hivyo kushindwa kununua vitoweo.
Akizungumza
kwa niaba ya wachuuzi wa samaki wa Deep See, Mohamed Ally amesema mazingira
yaliyopo sirafiki kwa afya za watumiaji eneo hilo, hata hivyo ameshangazwa na
kitendo cha wao kukatishwa leseni za kufanyia biashara ilihali hakuna huduma za
msingi wanazopata kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment