HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 29 May 2014

KALI YA MWAKA ALIYEZIKWA ATOKEA NYUMBANI KWAO NA KUELEZA MAKASA WA KUSISIMUA




Picha ya kwanza kushoto ni msichana Witness akiwa na wazazi wake baada ya kutokea nyumbani,(kulia)ni kaburi alilozikwa(chini)ni baadhi ya majirani waliohudhuria msiba wakifika kushudia Witness kurudi

Tukio la pekee ambalo linaonekana ni la kishirikina huko Arumeru/Arusha ni pale msichana Witness Obed ambaye inaelezwa alifariki na kuzikwa mara mbili ametokea nyumbani akiwa hai kwa wazazi wake na kisha kusimulia mkasa wa tukio ulivyomtokea. Mkasa huo ulitokea baada ya binti huyo kurudi toka chuo na kufika nyumbani saa mbili jioni akiwa amechelewa ndiyo iliyokuwa sababu ya kugombezwa na familia yake hasa babake mzazi.

Mzazi wake anasema alimgombeza, hivyo binti akatoroka. Binti huyo hakurudi na siku iliyofuata wakatoa tangazo la kumtafuta kupitia vyombo mbalimbali vya habari na sheria. Baadaye walisikia katika kijiji kingine walimwokota msichana aliyefariki. Walipoenda kuuliza waliambiwa alishazikwa.

Wakaenda kuomba kibali polisi cha kufukua kaburi ili kubaini kama ni binti yao, baada ya kupata kibali na kufukua kaburi waliitambua maiti kutokana na alama ambazo aliwa nazo wakati akiwa hai. Wakauchukua mwili huo na kwenda kufanya matanga kwao na kuuzika upya kwenye kaburi jingine.

Baada ya kuondoka alifika kwenye nyumba moja na kumkuta mama mmoja, aliomba maji ya kunywa. Alipewa na alipokuwa anakunywa mama yule alikuwa anamsimamia, lakini alipoonja na kuona machungu alikataa, lakini mama yule alimlazimisha kwa kumnywesha hadi akamaliza kisha akapoteza fahamu na hakujua nini kinaendelea na wapi aliko hakujitambua.

Anasema baadaye hajitambui amefikaje nyumbani, na mama yake alipomwona mara ya kwanza akifika alikimbia kufikiria anaona mzuka. Lakini baadaye alijipiga moyo konde na kumjongea binti yake.

Kuna matukio kadhaa yametokea siku za karibu huko kanda ya Ziwa na kwingineko kwa matuko kama haya, kuna kila dalili ya mchezo wa kishirikia.

Polisi wamesema wanataarifa juu ya tukio hilo na wanalifanyia uchunguzi wa kina.

No comments:

Post a Comment