| Watembeleaji wa maonesho hayo wakipata maelezo katika moja ya mabanda ya Biashara yaliyoko katika maoneshi hayo |
Halmashauri ya
jiji la Tanga imetoa wito kwa wakazi
wake kupitia maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano mkoani hapa kuwa
wananchi wapate kutembelea banda lao ili waweze kupata taarifa sahihi kuhusu
mji wa Pongwe pamoja na mambo ya usafi wa Mazingira.
Hayo yamesemwa
na mwoenyeshaji wa maonesho haya kwa niaba ya halmashauri Juma Mkombozi wakati
akizungumza na mtandao huu viwanjani
hapo kuhusu utoaji wa huduma yao kwenye maonyesho hayo ya kimataifa .
Aidha amesema
kuwa lengo la wao kushiriki kwenye maonesho ni kueleza kazi zao
na shughuli zote za halamashauri kwa wananchi ili wapate ufafanuzi juu ya mambo ambayo hawayafahamu .
Akielezea
shughuli za halmshauri amesema kuwa ni pamoja na fursa
na maeneo ya uwekezeji yliyopo ktika jiji la Tanga na kutolea ufafanuzi wa
shughuli za wadau wa maendeleo ya
jiji.
Sanjari na
hayo amesema wakazi wa jiji la hawana budi kutambua kuwa halmshauri inendelea kufanya jitihada zake kufanikisha
kuwa Tanga Televisheni itaanza kutumika baada ya muda mfupi hivyo
wananchi wameombwa kuwa na subira.
No comments:
Post a Comment