![]() |
| MBUNGE WA JIMBO LA BUMBULI MH.JANUARI MAKAMBA |
SERIKALI
imetakiwa kufikia uamuzi wa haraka juu ya kumtafuta mwekezaji mwingine wa
kiwanda cha Chai, cha Mponde, kilichopo Halmashauri ya Bumbuli,
Wilayani Lushoto, ili kuinusuru chai ya wakulima inayoendelea kuharibikia
shambani kwa miezi minane sasa, tangu kifungwe.
Kiwanda hicho cha Mponde ambacho ni Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA), wanamiliki asilimia hamsini, huku mwekezaji asilimia iliyobaki, kilifungwa baada ya wakulima kugoma kupeleka majani mabichi kwa madai kuwa mwekezaji huyo anawalangua.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani Bumbuli, wakulima hao
walisema tangu kiwanda hicho kimefungwa jana chai yao inaharibikia mashambani
na kuwapa ugumu wa maisha.
Hamis Jabiri mkulima wa Chai katika halimashauri hiyo, aliiomba serikali kuwafungulia kiwanda chao ili kunusuru maisha yao, maana wamekuwa wakiishi maisha magumu na kuongeza makali ya maisha na kuyumbisha uchumi wao.

Naye Robart Tembe, alisema baada ya kufikia uamuzi wa kukifunga
kiwanda hicho, serikali iliunda tume ili kupendekeza kuundwa kwa uongozi wa
muda katika kiwanda hicho.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Bumbuli, Beatreace Msomisi, alisema tangu kiwanda hicho
kilivyoacha kufanya kazi halmashauri hiyo imeathirika kiuchumi, kwasababu ya
kiwanda hicho kuwa tegemezi la wakulima.

No comments:
Post a Comment