![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa ameitaka jamii na wadau
wote wa shule ya Secondari Tanga Ufundi
(Tanga Tech)kufika kwenye mkutano utakao fanyika tarehe 15-3-2014 katika ukumbi
wa shule hiyo kuanzia majira ya saa nne kamili asubuhi.
Galawa ameyasema
hayo wakati akizungumza na
kituo hiki ofisini kwake na kusema kuwa lengo la mkutano huo ni
kuwakutanisha wanafunzi wote waliowahi
kusoma katika shule hiyo,walimu
waliowahi kufundisha katika shule hiyo pamoja na wadau wote washule hiyo
ili kuweza kujadili jinsi yakufanya maboresho ya shule hiyo kongwe na
kuiwezesha kuwa na miundombinu ya kisasa ya kujifunzia na kufundishia.
Pia
Galawa amesema kuwa jumla ya gharama yote ya miundombinu ni bilionii
mbili , milioni 460 laki 6 sitini Elfu na mia6 ambapo awamu yakwanza ya ukarabati inagharimu
sh bilioni
1,milioni 400 laki 8 hamsini na sita Elfu na mia sita na awamu ya
pili inagharimu kiasi cha sh bilioni 1, 59 milioni laki 7 na Elfu
hamsin.
Sambamba
na hayo amesema kamati ndogo ya maandalizi imesha pokea msaada wa mifuko 500 ya
saruji kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanga
cement na shilingi milioni 5 kwa ajili ya ununuzi wa nondo kutoka kwa
Mkurugenzi wa Steel rolling industry Tanga nakusema kuwa msaada huo umewezesha
kazi ya ujenzi ya uzio wa shule hiyo ianze na mpaka sasa msingi wa ukuta umesha
anza kuchimbwa.
Hata
hinyo Galawa amemalizia kwa kuwashukuru wadau wote walio changia na wale walio
anza kutuma salamu za udhibitisho wa
ushirikiwao katika mkutano huo utakaofanyika Shuleni hapo.

No comments:
Post a Comment