![]() |
| Kiwanda Cha Tanga Cement cha jijini Tanga ni miongoni mwa Viwanda vyikubwa ninavyoweza kuathirika kutokana na matatizo ya Umeme mkoani hapa |
Baadhi ya kampuni na wamiliki wa viwanda mkoani Tanga, wameingiwa na hofu ya kupungua kwa kasi ya uzalishaji wa bidhaa za viwandani, kufuatia kutokuwepo umeme wa uhakika na ukataji holela wa huduma hiyo.
Hayo yalielezwa jana katika kongamano la wadau wa watumiaji wa umeme Kanda ya Kaskazini, lililofanyika mjini hapa na kuelezwa kuwa, ili kuwavuta wawekezaji wa ndani na nje, Serikali ilipatie ufumbuzi tatizo la umeme.
Walisema kutokuwepo kwa umeme wa uhakika ni chanzo cha uzalishaji mdogo wa bidhaa viwandani, jambo linalochangia kupunguza wafanyakazi wa viwandani.
Ilielezwa Serikali imekuwa ikikosa mapato kutokana na wawekezaji kushindwa kuzalisha bidhaa.
![]() |
| Mafundi wa Tanesco wakiwa katika Shughli zao Jijini Tanga |
| Meya wa Jiji la Tanga Omar Guledi (Mwenye shati la mistari) Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego(Mwenye Nguo Nyekundu) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa walipotembelea kituo cha Umeme wa Vianda hivi karibuni jijini Tanga |
| Kituo cha Umeme wa Viwandani kilichoko Jijini Tanga |


No comments:
Post a Comment