UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Raundi
ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO-MATOKEO:
[Kwenye
Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumatano
Machi 12
FC
Barcelona 2 Manchester City 1 [4-1]
Paris
Saint-Germain 2 Bayer 04 Leverkusen 1 [6-1]
++++++++++++++++++++++++++++++++++
![]() |
| Refa: Stephane Lannoy akimnyooshea kadi nyekundu Zabaleta |
BARCELONA
2 MAN CITY 1
Ndani
ya Dakika 20 za kwanza Barca, kupitia Neymar, walifunga Bao ambalo lilikataliwa
kwa Ofsaidi ambapo marudio yalionyesha Goli ni halali na pia kunyimwa Penati ya
wazi baada ya Messi kuchezewa faulo na Lescott.
Kipindi
cha Pili, Dakika ya 67, Lionel Messi alifunga Bao kwa Barca baada ya Difensi ya
City kujichanganya.
Kwenye
Dakika ya 67, City walibaki Mtu 10 pale Zabaleta alipopewa Kadi ya Njano ya
Pili alipolalamika kwa Refa kunyimwa kwao Penati wakati Pique alipomkabili
Dzeko ndani ya Boksi.
City
walisawazisha katika Dakika ya 89 kupitia Nahodha wao Vincent Kompany lakini
Barca wakapiga Bao la Pili katika Dakika za Majeruhi baada Andres Iniesta
kutumbia kwenye Boksi, kumhadaa Kipa Joe Hart na kumpasia Dani Alves aliewasha
kigongo.
Barca
wametinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 4-1.
VIKOSI:
BARCELONA: Valdes, Alves, Pique, Mascherano,
Alba, Busquets, Fabregas, Xavi, Iniesta, Messi, Neymar
Akiba:
Pinto, Song, Pedro, Alexis, Sergi Roberto, Adriano, Bartra
MAN
CITY: Hart,
Zabaleta, Kompany, Lescott, Kolarov, Fernandinho, Toure, Milner, Silva, Nasri,
Aguero
Akiba:
Pantilimon, Clichy, Boyata, Navas, Garcia, Dzeko, Negredo
Refa:
Stephane Lannoy (France)
PARIS
ST-GERMAIN 2 BAYER LEVERKUSEN 1
Bayer
Leverkusen walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 6 kupitia Sidney Sam na PSG
kusawazisha kwa Bao la Marquinhos Dakika 7 baadae.
Lakini
Leverkusen wangeweza kufunga Bao la Pili katika Kipindi cha Kwanza walipopata
Penati kufuatia rafu ya Jallet kwa Derdiyok ambayo Kipa wa PSG, Sirigu,
aliokoa vizuri Penati hiyo iliyopigwa na Rolfes.
Dakika
ya 54, Lavezzi aliipa PSG Bao la Pili na kufanya Gemu iwe 2-1 na PSG kusonga
Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 6-1.
VIKOSI:
PSG:
Sirigu,
Jallet, Marquinhos, Thiago Silva, Digne, Pastore, Cabaye, Rabiot, Cavani,
Ibrahimovic, Lavezzi
Akiba:
Douchez, Camara, Menez, Thiago Motta, Alex, Maxwell, Lucas Moura.
BAYER
LEVERKUSEN: Leno,
Donati, Wollscheid, Toprak, Guardado, Rolfes, Reinartz, Can, Sam, Derdiyok,
Castro
Akiba:
Lomb, Son, Kiessling, Hilbert, Boenisch, Brandt, Wagener.
Refa:
Ivan Bebek (Croatia)
UEFA
CHAMPIONZ LIGI
Raundi
ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye
Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa
za Bongo]
Jumanne
Machi 18
22:45
Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü [1-1]
22:45
Real Madrid CF v Schalke 04 [1-6]
Jumatano
Machi 19
22:45
BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45
Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
++++++++++++++++++++++++++++++++++
MARUDIANO
MATOKEO:
[Kwenye
Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumanne
Machi 11
Bayern
Munich 1 Arsenal 1 [3-1]
Atletico de Madrid 4
AC Milan 1 [5-2]

No comments:
Post a Comment