HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 12 March 2014

WANAFUNZI WILAYANI MKINGA MKOANI TANGA WASOMA CHINI YA MIKOROSHO KWA UHABA WA MADARASA




Hali halisi katika Baadhi ya Shule za Msingi Nchini(Picha hizi ni kutoka Maktaba hasihusiani na Habari Hii)

Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakikonge, wilayani Mkinga wanasomea chini ya miti ya mikorosho kutokana na kukosekana kwa madarasa shuleni hapo.
Shule hiyo yenye wanafunzi 450 ina madarasa mawili, walimu wanne na haina nyenzo muhimu za kufundishia tangu ilipoanzishwa mwaka 2009.
Akizungumza katika mahojiano na Waandishi wa Habari Diwani wa Kata ya Duga, Ali Ali, alisema wanafunzi wa shule hiyo walianza kusoma chini ya mti na mpaka sasa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tano wanasoma chini ya mti na darasa la sita na la saba tu ndio waliopo madarasani.

“Hii shule inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwamo ukosefu wa madarasa na walimu….walimu waliopo ni wanne tu na madarasa ni mawili tu na mwaka huu tuna  wanafunzi wa darasa la saba tangu shule ilipoanzishwa hatujui matokeo yatakuaje," alisema Ali. (UNAWEZA KUCHUKUA HII KAMA QUATATION)

Hata hivyo, wananchi wa Sweden kupitia mfuko wa Agape Charity, wametoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni6.8.
Mwakilishi wa Agape ni kwamba Charity, Clemeny Hongole, alisema vitabu hivyo ni vya masomo ya Kiswahili, Historia, Jiografia, Uraia, Stadi za kazi na kiongozi cha mwalimu kwa masomo yote.

No comments:

Post a Comment