| Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Seleman Liwowa |
Wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavijeshi
wamevamia mashamba ya wakulima wa vijiji mbalimbali vilivyopo Kata nane za
wilayani ya Kilindi na kuharibu mahindi.
Uharibifu wa wadudu hao umezua hofu ya kuibuka kwa baa la njaa wilayani hapa.
Wakizungumza katika mahojiano na wanahabari kwenye Kijiji cha Msente, kilicho Kata ya Mswaki, wilayani Kilindi wakati walipokuwa wakikabidhiwa vyeti vya kuzaliwa vilivyoratibiwa na shirika la World Vision Tanzania, baadhi ya wakulima walisema hatua hiyo imewaathiri kwa kuwa wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
“Yaani viwavijeshi vimevamia mazao shambani kwa kiasi kwamba tumebaki na njaa...tunaomba sana serikali itusaidie kuondokana na uharibifu huu," alisema Daud Ramadhani, mkazi wa Msente.

Awali, kabla ya kukabidhi vyeti vya kuzaliwa, Mratibu
wa World Vision, Philipo Kibona, alisema kutokana na baadhi ya wakazi
kukabiliwa na uhaba wa chakula na wameathiriwa na tatizo hilo hawatatozwa fedha
za vyeti hivyo na badala yake fedha hizo ziwasaidie kununua chakula.
“Kutokana na uhaba wa chakula uliowakabili wananchi hawa tumeamua kutoa bure vyeti hivyo ili ziwasaidie kununua chakula," alisema Kibona.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Seleman Liwowa, akizungumza
na Waandishi wa Habari alikiri kuwa wadudu hao wameathiri mazao wilayani humo
na kwamba idara ya kilimo imeomba lita 1,000 za dawa za kuulia wadudu hao
kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ingawa wamefanikiwa kupata lita
200 tu ambazo wamezisambaza kwa baadhi ya vijiji ili kupunguza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment