![]() |
|
Kikosi cha Yanga. Kutoka kushoto waliosimama,
Dida,Msuva,Kiiza,Joshua,Yondani,Okwi. Kutoka kushoto walio chuchumaa,
Niyonzima,Twite,Cannavaro,Domayo na Ngassa
|
UONGOZI
wa Yanga SC umesema kwamba Sh 100,000 walizopewa kila mchezaji baada ya mechi
dhidi ya Al Ahly ya Misri Jumamosi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilikuwa ni
posho za mafuta ya gari zao, lakini usiku wa leo watapelekewa posho nzuri baada
ya ushindi wa 1-0 siku hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro amesema kuwa anashangazwa na madai ya wachezaji hao kwamba wamepewa posho kiduchu wakati ukweli ni kwamba walipewa fedha kwa ajili ya mafuta ya gari zao.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro amesema kuwa anashangazwa na madai ya wachezaji hao kwamba wamepewa posho kiduchu wakati ukweli ni kwamba walipewa fedha kwa ajili ya mafuta ya gari zao.
“Sisi tuna utaratibu wetu tuliojiwekea
kwa ajili ya hatua hii na wachezaji wetu watafurahi sana baada ya mechi ya
marudiano iwapo wataitoa Al Ahly, siku ile tuliwapa fedha kidogo kama posho ya
mafuta ya gari zao, kwa sababu walipewa mapumziko ya siku mbili kabla ua kurudi
kambini,”alisema Katabaro.
Aidha,
Katabaro alisema kwamba uongozi wa Yanga SC jioni ya leo utawapelekea posho
nzuri wachezaji wake waliopo kambini hoteli ya Bahari Beach, wakati donge nono
linawasubiri baada ya mchezo wa marudiano, wakifanikiwa kuwatoa mabingwa hao wa
Afrika.
Pamoja na hayo, habari zaidi kutoka ndani ya Yanga SC, zinasema kwamba wachezaji wote wa klabu hiyo, leo wamelipwa mishahara yao ya Februari- hivyo wataondoka kesho kwenda Misri wakiwa vizuri.
Pamoja na hayo, habari zaidi kutoka ndani ya Yanga SC, zinasema kwamba wachezaji wote wa klabu hiyo, leo wamelipwa mishahara yao ya Februari- hivyo wataondoka kesho kwenda Misri wakiwa vizuri.
Hivi karibuni baaadhi ya wachezaji wa Yanga SC walinukuliwa na wanahabari wakilalamika morali yao imeshuka kuelekea mchezo wa marudiano na Al Ahly ya Misri Jumapili hii mjini Cairo kuwania kutinga Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu wamepewa posho kiduchu baada ya mchezo wa kwanza Jumamosi walioshinda bao 1-0.
Lakini juzi, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza mapato ‘yaliyogunwa’ kutokana na idadi ya watu kuwa wengi na viingilio vilikuwa vikubwa.
TFF ilisema mechi hiyo ya Yanga dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa wa Afrika iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliingiza Sh. 448,414,000.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka kesho Dar es Salaam kwenda Cairo tayari kwa mchezo huo wa marudiano Jumapili.
![]() |
| OKWI AKIWAHENYESHA WAARABU |
KATIKA
HATUA NYINGINE
Beki
wa Al- Ahly, Said Ahmed Shedid amesema mechi ya marudiano itakuwa ngumu kwao
kutokana na kasi ya washambuliaji wa Yanga pamoja na uwezekano wa mechi hiyo
kuchezwa nje ya Cairo na El Gouna.
Yanga
na Ahly zitashuka uwanjani Jumapili hii kuumana katika pambano la marudiano la
Ligi ya Mabingwa Afrika raundi ya kwanza.
Beki
huyo Shedidin alisema pamoja na kubadilishwa uwanja huo bado wanategemea kupata
ushindani mkali kutoka kwa washambuliaji wa Yanga wenye kasi kubwa katika
kushambulia.
Alisema
mechi hiyo itakuwa ngumu kwao kama itachezwa nje ya Cairo na El Gouna, ambako
hali yake ya hewa inafanana na ile ya Tanzania.
Kutokana
na vurugu zilizojitokeza kwenye fainali ya Kombe la Super Cup kati ya Al-Ahly
na CS Sfaxien na kusababisha polisi 22 kuumia, mechi hizo zitachezwa bila
mashabiki.
Serikali
ya Misri imesema mechi zote za Cairo zitachezwa bila ya mashabiki au kucheza
kwenye Uwanja wa Jeshi wa jijini Cairo.
Naye
nahodha Mohammad Yousuf, akiuzungumzia mchezo huo wa Jumapili alisema mabingwa
hao wa Tanzania wameoneka kuwa wazuri zaidi katika kushambuliajia kwa kasi na
kujilinda.
"Nidhamu
na kasi yao wanapokuwa na mpira ni jambo inabidi kulifanyia kazi ya ziada kabla
ya mechi yetu ya marudiano."
Yousuf
alifafanua kuwa mechi hiyo haitakuwa rahisi kwao kutokana na uchezaji wa
wapinzani wao. Lakini kurejea kwa nyota wao kama Abdullah Saeed na Sherif
Abdul-Fadil ni faida kwao.
Tayari
CAF imeshamtangaza mwamuzi wa Badara Diatta kuchezesha mchezo huo akisaidiwa na
Jay Haji Abdul Aziz, na Bangor Forbade, na mwamuzi wanne Kebbi Dauda, na
msimamizi wa mchezo huo atakuwa Massa Diarra kutoka Mauritania.
Wakati huohuo; Serikali imeitoa
hofu Yanga kwa kusema kwamba tayari imechukua hadhari ili kuhakikisha inakuwa
salama muda wote itakapokuwa Misri kwa ajili ya pambano dhidi ya Al Ahly.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe akizungumza jijini
Dar es Salaam alisema, wizara yake imefanya mawasiliano na Balozi wa Tanzania
nchini Misri kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa msafara wa Yanga.
"Nichukue
fursa hii kusema kwamba serikali ipo nyuma ya Yanga kwa kuhakikisha inakuwa
salama muda wote itakapokuwa Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Al
Ahly.
"Tayari
wizara yangu imewasiliana na balozi wetu Misri. Watapewa ulinzi mkali na wa
hali ya juu kuanzia mazoezini hadi hotelini,"alisema Membe.
Aliongeza:"Lengo
ni kuhakikisha timu yetu haifanyiwi vioja au vituko vya aina yoyote itakapokuwa
kule, tunataka icheze mechi ikiwa huru."
Tayari
uongozi wa Yanga umethibitisha kwamba msafara wa timu hiyo utaondoka nchini
kesho kwa ndege ya kuekelea Misri tayari kwa ajili ya mchezo wao.


No comments:
Post a Comment